• HABARI MPYA

    Wednesday, December 26, 2012

    MIENO, ATUDO WAREJEA KENYA

    Atudo

    Na Mahmoud Zubeiry
    BEKI Joackins Atudo na kiungo Humphrey Mieno wamebaki nyumbani kwao Nairobi, Kenya na watajiunga tena na kikosi cha Azam FC, baada ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.
    Wawili hao, walikuwepo kwenye kikosi cha Azam kilichotwaa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumamosi iliyopita, wakiwachapa wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
    Ikiwa njiani kurejea Dar es Salaam, Meino na Autdo waliteremka Nairobi wakati mabingwa hao wa Kombe la Hisani wakiwasili Tanzania usiku wa saa 7:00 jana.
    Katibu wa Azam, Nassor Idrisa amesema wachezaji wengine pia watapewa mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya sikukuu ya Krisimasi na baada ya hapo watakutana kujiandaa kwa safari ya Zanzibar kwenda kutetea Kombe lao la Mapinduzi.
    Azam Jumamosi ilitwaa ubingwa wa Kombe la Hisani baada ya kuwafunga wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa.
    Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75 na katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
    Azam iliingia fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
    Kikosi cha Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
    Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MIENO, ATUDO WAREJEA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top