• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 20, 2012

  MTANZANIA KUWANIA UBINGWA WA MADOLA NDONDI ZA KULIPWA

  Fadhil Majia

  Na Prince Akbar
  BODI ya Wakurugenzi ya Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) imepiga kura kumruhusu bondia wa Tanzania Fadhili Majia apambane na bondia  Isaac Quaye wa Ghana katika mchujo (Elimination) wa kutafuta mpinzani atakayekutana na bingwa wa mkanda wa Jumuiya ya Madola katika uzito wa Fyweight Kevin Satchell wa Uingereza. Mpambano wa Fadhili Majia na Isaac Quaye utafanyika jijini Accra, Ghana tarehe 22, Febryary 2013.
  Rais wa TPBC Onesmo Ngowi ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya Baraza la Ngumi la Jumuiya ya madola na alikuwa wa kwanza kumpigia bondia Fadhili Majia kura ili acheze na Quaye.
  Hii itakuwa mara ya kwanza kwa bondia Fadhili Majia kugombea mkanda wa Jumuiya ya Madola ambayo inaziunganusha nchi zote zilizokuwa zinatawaliwa na himaya ya Kiingereza.
  Wakati huo huo Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola imepitisha azimio la kuruhusu ubingwa wa baraza hilo katika bara la Afrika. Ubingwa huo utakuwa unajukikana kama “CBC Africa Zone” na tayari wapo mabondia kadhaa wa nchi za Afrika ya Magharibi ambao wameshandaa mapambano mwakani.
  Napenda kuwahamasisha mapromota wa Kitanzania kuchangamkia fursa hizi adimu na kuandaa mapambano ya ubingwa wa "CBC Africa Zone" kwa manufaa ya mabondia wetu.
  TPBC imejiandaa kuwatafutia mabondia wa Kitanzania mapambano mengi ya nje ili waweze kujijenga kimchezo na pia kuweza kupata kipato kizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MTANZANIA KUWANIA UBINGWA WA MADOLA NDONDI ZA KULIPWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top