Rais wa TFF, Leodegar Tenga |
Na Prince Akbar
MICHUANO ya
Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
Michuano hiyo,
ambayo hudhaminiwa na Azam, watengenezaji na wasambazaji wa maji ya Uhai, inatarajiwa
kufikia tamati Desemba 22 mwaka huu.
Ofrisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN
ZUBEIRY mjini hapa kwamba, wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni
wale tu ambao usajili wao umefanyika TFF na kupatiwa leseni.
“Hakutakuwa
na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu. Taratibu
zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya
michuano hiyo,”alisema ‘Big Bon’.