SOURCE: FULL SHANGWE
Mkurugenzi mkuu wa City Sports Lounge Bw. Juma Pinto akiongea na Tume Makani pamoja na Mkewe wakati walipohudhuria kwenye uzinduzi wa klabu hiyo iliyopo maeneo ya Posta jijini Dar es salaam, klabu hiyo ni maalum kwa kuonyesha michezo hasa mpira wa miguu kupitia Luninga ya Supersports inayotumia ving'amuzi vya DSTV.
Watu wengi wamehudhuria katika hafla hiyo na sasa hivi wanaagalia mchezo wa fainali kati ya timu ya Chealsea ya Uingereza na Bayern Munchen ya Ujerumani unaochezwa kwenye uwanja wa Alianz Arena jijini Munichen usiku huu.
Hapa John Bukuku, Mkurugenzi wa Full Shangwe kulia akikipata mawili matatu kutoka kwa Ridhiwani Kikwete. . Kushoto ni Makamu wa kwanza wa rais wa TFF, Athumani Nyamlani.
Wadau mbalimbali wakiwa katika klabu hiyo usiku huu ili kujionea mchezao kati ya Chealsea na Bayern Munichen.
Mdau Grace wa NHIF na Laitness Sirikwa wakijiachia klabu City Sports Lounge.
Wadau wakisubiri mchezo huo.
Ridhiwan Kikwete akisalimianha na mdau wa soka Jerry Koto katikati ni Makamu wa kwanza wa Rais Athman Nyamlani
Wadau wakisubiri mchezo huo kwa hamu.
Baraka Shelikindo na wadau wengine wakijimwaga klabuni hapo usiku huu.
Kutoka kulia ni Rajab KatundaRidhiwan Kikwete, Juma Mabakila, Muddy El-maamry na
Vimwana waliowahi kushiriki Miss Tanzania enzi hizo, Lucy Kihwele kulia na Miriam Ikoa kushoto walikuwepo pia.
MC wa sherehe hiyo Gardiner G Habash akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa utaratibu wa sherehe hiyo.
Kutoka kulia ni Eddo, Konoki na Juma Pinto wakishoo Love.
Juma Pinto kushoto na mpenzi maarufu wa Simba, Evance Aveva aliyekuwa Meneja wa iliyokuwa Embassy Hotel, wakijadili jambo wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo.
Juma Pinto akishoo Love na wageni wake waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi usiku huu.
Watu mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo wakipata kinywaji na kuzungumza mawili matatu katika hafla hiyo.
SOURCE: FULL SHANGWE
SOURCE: FULL SHANGWE













.png)
0 comments:
Post a Comment