// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WACHEZAJI, MAKOCHA TAIFA STARS KUGAWANA DOLA 10,000 ZA COSAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WACHEZAJI, MAKOCHA TAIFA STARS KUGAWANA DOLA 10,000 ZA COSAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Friday, August 04, 2017

  WACHEZAJI, MAKOCHA TAIFA STARS KUGAWANA DOLA 10,000 ZA COSAFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE Shirikisho la Soka kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA), limekabidhi zawadi ya dola 10,000 za Kiamrekani kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufuatia timu yake ya taifa ya wakubwa, Taifa Stars kushinda nafasi ya tatu katika mashindano ya COSAFA Castle Juni mwaka huu mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
  Fedha hizo ni sawa na Sh. 22,000,000 ambako TFF, imeamua wagawane sawa benchi la ufundi na wachezaji wote walioshiriki michuano hiyo.
  Kadhalika COSAFA imetuma fedha za zawadi kwa wachezaji wa Tanzania walioshinda tuzo Mchezaji Bora wa Mechi mbalimbali za michuaano hiyo.
  Elias Maguri alikuwa mchezaji bora katika mechi dhidi ya wenyeji, Afrika Kusini na akifunga na bao pekee la ushindi wa 1-0
  Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi; Muzamil Yassin aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola; Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
  Mwingine ni Kipa Bora wa michuano hiyo, Said Mohammed aliyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili baada ya kuifunga Lesotho kwa penalti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI, MAKOCHA TAIFA STARS KUGAWANA DOLA 10,000 ZA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top