• HABARI MPYA

  Friday, August 04, 2017

  KELECHI IHEANACHO ASAINI MIAKA MITANO LEICESTER CITY

  KLABU ya Leicester City imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Mnigeria Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25 akisaini mkataba wa miaka mitano.
  City imepewa nafasi ya kumnunua tena kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 50 mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye anaweza kuichezea Foxes kwa mara ya kwanza leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Borussia Monchengladbach.
  Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria ambaye atavaa jezi namba  8 amesema: "Najisikia vizuri na nina furaha kuwa sehemu ya timu hii. Nafahamu malengo ya timu na katika mazungumzo na kocha amenijulisha nini ninatakiwa kufanya kuisaidia timu kupata inacokitaka. Nimeshawishika na ninafuraha kuwa hapa," amesema.

  Leicester City imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Mnigeria, Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Kocha wa Leicester, Craig Shakespeare amemtaka Iheanacho, aliyefunga mabao 12 katika mechi 46 za Ligi Kuu ya England akiwa na Man City kuongeza bidii ili kuisaidia timu yake mpya, naye pia awe mmoja wa washambuliaji hatari duniani.
  Iheanacho alijiunga akademi ya Manchester City kama mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 Januari 10 mwaka 2014 kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2015.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KELECHI IHEANACHO ASAINI MIAKA MITANO LEICESTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top