• HABARI MPYA

  Thursday, August 03, 2017

  SIMBA SC YATOA SARE 1-1 NA MABINGWA WA AFRIKA KUSINI, BIDVEST

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini, Bidvest Wits katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Sturrock Park, Chuo Kikuu cha Afrika Kusini asubuhi ya leo.
  Katika mchezo huo wa kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya, Simba SC walikuwa wa kwanza kupata bao, lililofungwa na beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni dakika ya 33 kabla ya wenyeji kusawazisha.
  Kocha Mcameroon wa Simba, Joseph Omog akizungumza na wachezai wake
  Kiungo Mohammed 'Mo' Ibrahim akiwapindua wachezaji wa Bidvest leo

  Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kirafiki wa Simba katika kambi yake Afrika Kusini kujiandaa na msimu, baada ya Jumamosi kufungwa 1-0 Orlando Pirates.
  Baada ya mchezo huo, Simba SC inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya mchezo mwingine wa kujipima nguvu dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar  es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOA SARE 1-1 NA MABINGWA WA AFRIKA KUSINI, BIDVEST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top