• HABARI MPYA

  Thursday, August 03, 2017

  NEEMA ZAIDI YAMIMINIKA SINGIDA UNITED, YARA NAO WAWEKA MILIONI 250

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Singida United imeingia mkataba wa udhamini na kampuni ya uzalishaji wa mbolea, YARA wa zaidi ya Sh. Milioni 250 kwa mwaka mmoja.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo kwenye Hafla iliyofanyika ukumbi wa Kivukoni, uliopo ndani ya hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa klabu hiyo, Sanga Festo amesema kwamba udhamini huo mpya habari njema za kiuchumi kwa klabu yao.
  “Tuna furaha  kutangaza kuingia mkataba wa udhamini na YARA kwa mwaka mmoja, haya ni manufaa makubwa sana katika klabu yetu na hadi sasa tuna hekari 10 kwa ajili ya  kilimo cha zao la alizeti chini ya usimamizi wa kampuni ya YARA, itakayosimamia suala zima la kilimo,”amesema Sanga.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa YARA, Alexandre Macedo amesema kwamba wamefurahi kuwa sehemu ya Singida United na watayaboresha mahusiano hayo katika sekta ya kilimo.
  Singida United imepanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwaka huu tangu iteremke mwaka 2002, lakini imekuja na ngekewa ya kuoata udhamini mnono kutoka kampuni za SportPesa, Puma, Oryx na sasa YARA.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEEMA ZAIDI YAMIMINIKA SINGIDA UNITED, YARA NAO WAWEKA MILIONI 250 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top