• HABARI MPYA

  Tuesday, August 01, 2017

  SIMBA SC YAGONGWA ‘KIMOKO’ AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIGOGO wa soka Tanzania, Simba SC leo wame wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu katika kambi yao ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Orlando Piates mjini Johannesburg.
  Kwa mujibu wa Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara, Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog ilicheza vizuri pamoja na kufungwa.
  Kipa mpya wa Simba, Aishi Manula (kulia) kutoka Azam FC akiwa kambini Afrika Kusini
  “Kwa mujibu wa maelezo ya benchi la Ufundi, mchezo ulikuwa mzuri na timu ilicheza vizuri, lakini bahati ilikuwa wenyeji Pirates kupata ushindi huo.
  Manara alisema Omog anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja aliwapa nafasi karibu wachezaji wote leo kucheza, akipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi.
  Simba inatarajiwa kushuka tena dimbani Alhamisi kumenyana na mabingwa wa Afrika Kusini, Bidvest Wits kabla ya kurejea Dar es Salaam tayari kwa mchezo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwenye tamasha la Simba Day.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAGONGWA ‘KIMOKO’ AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top