• HABARI MPYA

  Friday, August 11, 2017

  SIMBA SASA KUMENYANA NA MTIBWA SUGAR JUMAPILI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba itamenyana na Mtibwa Sugar ya Morogoro Jumapili Uwanja wa Tai,a Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Yanga SC Agosti 23, mwaka huu.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba, baada ya kushindikana kucheza na Singida United, sasa watamenyana na Mtibwa Sugar. 
  Pamoja na kujipima kabla ya kumenyana na Yanga, Manara pia amesema kwamba mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. 
  Manara amesema baada ya mchezo huo, kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kitavuka bahari ya Hindi kwenda visiwa vya Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii.
  Wakati huo huo; Simba leo imecheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya timu ya Polisi Dar es Salaam na kushinda 2-1 Uwanja wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi Polisi, Kurasini, Jijini mabao yake yakifungwa na Laudit Mavugo na Mwinyi Kazimoto.
  Huo unakuwa mchezo wa nne wa kirafiki kwa Simba ikiwemo miwili iliyocheza katika ziara yake ya Afrika Kusini ambako ilifungwa 1-0 na wenyeji Orlando Pirates kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Bidvest na Jumanne wiki hii ilishinda 1-0 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Uwanja wa Taifa, bao pekee la Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, pasi ya Emmanuel Okwi.
  Kocha Mcameroon wa Simba Sports Club, Joseph Marius Omog anataka mchezo mmoja zaidi wa majaribio kabla ya kukutana na mahasimu wa jadi, Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SASA KUMENYANA NA MTIBWA SUGAR JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top