• HABARI MPYA

  Saturday, August 12, 2017

  NINJA AJIFUNGA, YANGA YALALA 1-0 KWA RUVU CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepoteza mchezo wa kirafiki jioni ya leo baada ya kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ alimfunga kwa kichwa cha mkizi kipa wake, Ramadhan Awam Kabwili dakika ya 22 wakati akijaribu kuokoa krosi ya Shalla Juma kutoka upande wa kushoto wa Uwanja kuipatia bao pekee la ushindi Ruvu.
  Abdallah Hajji ‘Ninja’ amejifunga leo Yanga ikichapwa 1-0 na Ruvu Shooting Chamazi 

  Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima nguvu kwa Yanga inayofundishwa na kocha Mzambia, George Lwandamina baada ya Jumamosi iliyopita kushinda 3-2 dhidi yas Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na baada ya matokeo hayo, Yanga SC itaondoka Dar es Salaam mapema kesho kwenda Zanzibar ambako usiku watamenyana na Mlandege Uwanja wa Amaan katika mchezo mwingine wa kirafiki.
  Mapema Jumatatu Yanga watakwenda kisiwani Pemba kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba Agosti 23 Uwanja wa Taifa. 
  Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Hassn Kessy/Juma Abdul, Gardiel Michael, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Vincent Andrew/ISSAMnigeria, Said Juma ‘Makapu’/Maka Edward, Pius Buswita/Said Mussa, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Hajib/Raphael Daudi na Emmanuel Martin.
  Ruvu Shooting; Bidii Hussein/Abdallah Rashid, Said Madega/Abdallah Mpambika, Yussuf Nguya, Frank Msese, Mangasini Mbonosi, Baraka Mtuwi/Chande Magoja, Jamal Soud/William Patrick, Shaaban Msala, Shalla Juma/Issa Kanduru, Fully Maganga na Khamis Mcha ‘Vialli’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NINJA AJIFUNGA, YANGA YALALA 1-0 KWA RUVU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top