• HABARI MPYA

  Thursday, August 03, 2017

  NEYMAR KILA KITU SAFI KUSAINI PSG KWA DAU LA REKODI LA DUNIA

  Nyota Mbrazil wa Barcelona, Neymar anakaribia kuhamia Paris Saint-Germain kwa ada ya Pauni Milioni 198 PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  WACHEZAJI 10 GHALI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI 

  1) Neymar (Barcelona kwenda PSG, 2017) - Pauni Milioni 198
  2) Paul Pogba (Juventus kwenda Man United, 2016) - Pauni Milioni 89.3
  3) Gareth Bale (Tottenham kwenda Real Madrid, 2013) - Pauni Milioni 85.3
  4) Cristiano Ronaldo (Manchester United kwenda Real Madrid, 2009) - Pauni Milioni 80
  5) Gonzalo Higuain (Napoli kwenda Juventus, 2016) - Pauni Milioni 75.3
  6) Neymar (Santos kwenda Barcelona, 2013) - Pauni Milioni 75.2
  7) Romelu Lukaku (Everton kwenda Manchester United, 2017) - Pauni Milioni 75
  8) Alvaro Morata (Real Madrid kwenda Chelsea, 2017) - Pauni Milioni 70.6
  9) Luis Suarez (Liverpool kwenda Barcelona, 2014) - Pauni Milioni 65
  10) James Rodriguez (Monaco kwenda Real Madrid, 2014) - Pauni Milioni 63 
  NYOTA Mbrazil wa Barcelona, Neymar amewasili Jijini Paris kukamilisha uhamisho wake klabu ya Paris Saint-Germain kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 198.
  Neymar anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 596,000 kwa wiki baada ya kodi na dau la kusaini mkataba Pauni Milioni 45.
  Kwa ujumla, dili zima litaigharimu PSG kiasi cha Pauni Milioni 398.
  Tetesi za Neymar kuondoka Barcelona zilianza kuvunja taratibu kwenye vyombo vya Habari, ingawa mwanzoni klabu ya Hispania ilikanusha na kusema mchezaji huyo hataondoka.
  Lakini hawakujua kama kulikuwa kuna mazungumzo ya siri kati ya baba yake Neymar na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi aliyekuwa akimtafutia mkataba mpya mwanawe.
  Lakini Jumatano asubuhi mambo yakaanza kuwa hadharani, baada ya Neymar kwenda kwenye mazoezi ya Barcelona na kutumia dakika 40 kukutana na Wakurugenzi wa klabu na kuwaaga wachezaji wenzake.
  Kisha Barcelona ikatoa taarifa muda wa chakula cha mchana ikithibitisha kwamba Neymar ameomba kuondoka ili akakamilishe uhamisho wake PSG.
  Jumatano usiku, wakala Wagner Ribeiro, ambaye anafanya kazi za mikataba ya Neymar, akathibitisha ada italipwa ndani ya saa 48 zijazo na mchezaji anaweza kutambulishwa mjini Paris mapema Ijumaa.
  Hakukuwa na hotuba ya maana wakati Neymar anaaga kwenye chumba cha kubadilishia nguo, zaidi ya kuagana na wachezaji wenzake mmoja baada ya mwingine. 
  Baadaye nyota mkubwa zaidi wa klabu hiyo, Muargentina Lionel Messi akaposti kwenye mtandao wa kijamii: "Ilikuwa babu kubwa kuwa nawe rafiki yangu Neymar kwa miaka yote hiyo. Nakutakia bahati nzuri katika hatua nyingine kwenye maisha yako,".
  Yote haya yanatokea miezi 10 tu tangu Neymar asaini mkataba mpya wa kuendelea kucheza Barcelona hadi mwaka 2021.
  Barcelona ilithibitisha haikumpa baba yake Neymar 'cha juu' wakati wa kusaini mkataba huo mpya, licha ya malipo ya Pauni Milioni 22 kufanywa Jumatatu na klabu hiyo inatarajia kufuata ushauri wa kisheria baada ya uhamisho wa mchezaji huyo kukamilika ili kujua kama malipo zaidi na wao watatakiwa kufanya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR KILA KITU SAFI KUSAINI PSG KWA DAU LA REKODI LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top