• HABARI MPYA

  Monday, August 14, 2017

  KADO APUMZISHWA SIKU TATU BAADA YA ‘KUJERUHIWA’ NA BOCCO JANA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIPA namba moja wa Mtibwa Sugar, Shaaban Hassan Kado atapumzika kwa siku tatu kuanzia leo kufutaia jana kuumia goti katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kado jana aliibua hofu baada ya kugongana na mshambuliaji wa Simba, John Raphael Bocco dakika ya 28 na kuondolewa uwanjani dakika mbili baadaye akichechemea huku akiugulia maumivu kufuatia kupatiwa matibabu ya awali.
  Hata hivyo, Meneja wa Mtibwa Sugar, Sidy Ibrahim ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Kado anaendelea vizuri na ataanza mazoezi baada ya siku tatu.
  Ibrahim amesema kwamba Kado amefanyiwa vipimo leo na kugundulika hajapata maumivu makali, hivyo amepewa mapumziko ya siku tatu.
  Shaaban Kado akiwa amelala langoni mwake baada ya kuumia goti jana kufuatia kugongana na John Bocco
  Ibrahim amesema majeruhi wengine wa timu hiyo ni viungo Hassan Dilunga na Haroun Chanongo, ambao wote wanasumbuliwa na maumivu madogo ya nyama za paja na wataanza mazoezi mwishoni mwa wiki, wakati mshambuliaji Stahmili Mbonde alikuwa anasumbuliwa na Malaria na ataanza mazoezi keshokutwa. 
  Kikosi cha Mtibwa Sugar baada ya kufungwa 1-0 jana na Simba, kimerejea Manungu, Turiani mkoani Morogoro leo kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo 1999 na 2000, wataanza kampeni yao ya kuwania taji la tatu la ligi hiyo kwa kumenyana na Stand United Agosti 26, Uwanja wa Manungu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KADO APUMZISHWA SIKU TATU BAADA YA ‘KUJERUHIWA’ NA BOCCO JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top