• HABARI MPYA

  Monday, August 14, 2017

  BEKI MGHANA ANUKIA LIGI KUU ENGLAND KUTOKA CHAMPIONSHIP

  KOCHA wa Barnsley, Paul Heckingbottom hawezi kumtumia Andy Yiadom anayetakiwa na Huddersfield Town kwa sababu yuko njia panda.
  Beki huyo Mghana mwenye umri wa miaka 25, aliyewasili kutoka timu ya Ligi Daraja la Pili, Barnet mwezi Mei mwaka 2016, aliachwa kwenye kikosi kilichofungwa nyumbani na Ipswich Jumamosi baada ya kuanzishwa katika mechi mbili zilizotanguli.
  Heckingbottom amesema mazungumzo na timu hiyo mpya ya Ligi Kuu yam England yanaendelea. "Machoni mwangu, simuoni Yids hadi nitakapoambiwa tofauti,"amesema.
  Andy Yiadom anatakiwa na timu mpya ya Ligi Kuu ya England, Huddersfield Town 

  "Haikuwa sahihi kwangu kumjumuisha Yids katika mchezo wa Jumamosi na ikiwa itabaki kama ilivyo, hatacheza na Jumanne pia kwa sababu haitakuwa vizuri kwa wachezaji wengine,".
  "Tunajiandaa kwa mchezo wetu na dhahiri Yids yuko njia panda kwa sasa. Hadi itakapojulikana moja na nikaambiwa, simfikirii," amesema.
  Heckingbottom amesema mazungumzo juu ya mchezaji huyo aliyecheza mechi 33 za Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship msimu uliopita yanaendelea,.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI MGHANA ANUKIA LIGI KUU ENGLAND KUTOKA CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top