// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BONDIA WA TANZANIA ASHINDA BOTSWANA NA KUTWAA TAJI LA WBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BONDIA WA TANZANIA ASHINDA BOTSWANA NA KUTWAA TAJI LA WBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, August 09, 2017

  BONDIA WA TANZANIA ASHINDA BOTSWANA NA KUTWAA TAJI LA WBA

  Na Mwandishi Wetu, GABORONE
  BONDIA chipukizi wa Tanzania, Mussa Mwakinyo (pichani kulia) jana amefanikiwa kutwaa la WBA Pan African uzito wa Super Welter, baada ya kumshinda kwa Technical Knockou (TKO) Anthony Jarmann wa Botswana mjini Gaborone, Botswana.
  Lilikuwa pambano kali, lililokutanisha mabondia bora na walijiandaa vizuri, ambao walipambana vikaki kwa raundi zote 10.
  Lakini dalili za Jarmann kupoteza pambano zilianza kuonekana raundi ya sita baada ya kuangushwa na ngumi kali ya Mtanzania. Hata hivyo, Jarmann aliinuka na kumalizia raundi, ingawa hata raundi ya saba alizidiwa pia.
  Jarmann akasimama imara katika raundi ya nane na kufanikiwa naye kumkalisha chini Mwakinyo ambaye mwishowe aliokolewa na kengele.
  Katika Raundi ya tisa, Mwainyo alitumia muda mwingi kumkimbia ulingoni Jarmann ulingoni, kabla ya kuingia kwa kasi raundi ya 10 na kumshambulia kwa ngumi mfululizo za aina zote mpinzani wake hadi refa aliposimamisha pambano.
  Matokeo hayo yanamaanisha Jaramann anavuliwa taji la WBA Pan African ambalo sasa linakwenda kuweka maskani eneo la Tangamano mkoani Tanga, anapotokea Mwakinyo.
  Baada ya ushindi huo, Mwakinyo anatarajiwa kurejea leo Dar es Salaam na moja kwa moja kuunganisha Tanga. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BONDIA WA TANZANIA ASHINDA BOTSWANA NA KUTWAA TAJI LA WBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top