• HABARI MPYA

    Saturday, June 01, 2019

    SAMATTA AWAFARIJI AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA KABLA YA MUDA MWANANYAMALA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Ally Samatta leo ametembelea hospitali ya Mwananyamala, Manispaa ya Kinondoni mjini Dar es Salaam na kutoa misaada ya vitu vidogo vidogo kwa akina mama ambao waliojifungua kabla ya wakati.
    Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubeligiji amefanya zoezi hilo kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation na miongoni mwa vitu alivyotoa ni sabuni aina ya Omo.
    “Nilifurahi kuona akina mama wakiwa wenye nyuso za furaha baada ya kuniona na wengi kufurahishwa na kitendo cha mimi kupita hospitalini hapa. Lakini pia nimebahatika kupanda miti ndani ya hospitali hii," amesema Samatta.
    Mbwana Samatta akikabidhi misaada ya vitu vidogo vidogo kwa akina mama ambao waliojifungua kabla ya wakati leo hospitali ya Mwananyamala

    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC amefanya hayo siku moja tu kabla ya mechi yake ya Hisani kesho katika tamasha la Nifuate, maalum kuchangia miundombinu ya shuke za Msingi Dar es Salaam.
    Samatta ameunda kikosi cha yeye rafiki zake ambao watamenyana na kikosi cha mwanamuziki nyota nchini, Ally Kiba na Rafiki zake kesho jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Hii itakuwa mara ya pili kwa Samatta kuungana na Kiba ambaye msimu huu ameichezea Coastal Union katika Ligi Kuu kufanya tamasha hilo baada ya mwaka jana – na fedha zilizopatikana zilikwenda kununulia madawati ya shule za Msingi. 
    Samatta amerejea nchini wiki iliyopita akitoka kuipa Genk ubingwa wa Ligi Kuu ya Ubelgiji huku naye akishinda tuzo yake Mwanasoka Bora Mwafrika anayecheza Jupiler Pro League baada ya kumaliza na mabao 23 msimu huu.
    Kwa ujumla, Samatta mwenye umri wa miaka 26, ameifungia Genk mabao 62 katika mechi 156 za mashindano yote tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Katika ligi ya Ubelgiji pekee amefunga mabao 47 katika mechi 123, kwenye Kombe la Ubelgiji amefunga mabao mawili katika mechi tisa na Europa League amefunga mabao 14 katika mechi 24.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AWAFARIJI AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA KABLA YA MUDA MWANANYAMALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top