• HABARI MPYA

    Thursday, June 20, 2019

    SPIKA NDUGAI ATEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS CAIRO KUWAPA MOTISHA VIJANA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amekutana jana na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars, katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.
    Katika mazungumzo na wachezaji hao, Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kuwataka vijana hao kupambana kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21,nchini Misri.
    Mheshimiwa Spika, aliwataka wachezaji  hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao wameyaelekeza kwao.

    Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta,alimuahidi Mheshimiwa Spika kuwa wamepokea salamu za Mheshimiwa Rais,na wamemuahidi kuwa wataingia uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.
    Alisema, hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi zote za makundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPIKA NDUGAI ATEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS CAIRO KUWAPA MOTISHA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top