• HABARI MPYA

    Sunday, June 23, 2019

    UGANDA YAFUTA GUNDU LA MIAKA 41 AFCON KWA KUIPIGA DRC 2-0

    UGANDA imepata ushindi wa kwanza kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 41 kufuatia kuichapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 2-0 kwenye mchezo wa Kundi A leo mjini Cairo.
    Mabao ya Uganda katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji wa KCCA ya nyumbani, Kampala Patrick Kaddu dakika ya 14 na mshambuliaji wa Simba SC ya Tanzania, Emanuel Okwi dakika ya 48 na wote wakimalizia pasi za kiungo wa Gorica ya Croastia, Farouk Miya.
    Mara ya mwisho The Cranes kushinda mechi AFCON ilikuwa ni Machi 1978 ilipoifunga Nigeria kwenye Nusu Fainali kabla ya kwenda kufungwa na wenyeji, Ghana kwenye fainali.

    Tangu hapo, Uganda haikufuzu tena kwenye AFCON hadi miaka miwili iliyopita nchini Gabon amnako matokeo yao mazuri kwenye kundi lao ilikuwa ni sare.
    Uganda sasa wanaongoza Kundi A baada ya ushindi wao wa leo, wakifuatiwa na wenyeji, Misri ambao jana waliifunga Zimbabwe 1-0. 
    Mechi nyingine za leo zilikuwa za Kundi B, Nigeria imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Burundi, bao pekee la mshambuliaji wa Shanghai Shenhua ya Chiba, Odion Jude Ighalo dakika ya 77.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YAFUTA GUNDU LA MIAKA 41 AFCON KWA KUIPIGA DRC 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top