Sunday, June 16, 2019

    AZAM FC NA MTIBWA SUGAR ZATINGA NUSU FAINALI YA LIGI KUU YA VIJANA U20

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya vijana ya Azam FC (Azam U-20) imetinga nusu fainali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20 Premier League) baada ya kuichapa Biashara United mabao 3-1 usiku huu.
    Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa kikosi hicho kwenye hatua ya nane bora ya michuano hiyo ikiwa Kundi B, ambapo mechi ya kwanza iliichapa Tanzania Prisons 2-0.
    Mabao ya Azam U-20 usiku huu yamefungwa na nahodha wa timu hiyo, Lusajo Mwaikenda, Abadi Kawambwa na Agiri Ngoda, aliyehitimisha ushindi huo.

    Mbali na Azam U-20, timu nyingine ya kundi hilo iliyofuzu nusu fainali ni Mtibwa Sugar, iliyoichapa Prisons 3-1 kwenye mchezo wa awali uliofanyika jioni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA MTIBWA SUGAR ZATINGA NUSU FAINALI YA LIGI KUU YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry