• HABARI MPYA

    Sunday, June 09, 2019

    KAGERA SUGAR NA MWADUI FC BADO TUPO NAZO LIGI KUU BAADA YA KUZIPIGA PAMBA NA GEITA GOLD PLAY-OFF

    Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
    TIMU za Kagera Sugar na Mwadui FC zimefanikiwa kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi kwenye mechi zao za leo za Play-Off dhidi ya Pamba SC na Geita Gold Mine za Daraja la Kwanza. 
    Uwanja wa Mwadui Complex wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Mwadui FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwadui.
    Kwenye mchezo huo, mabao ya Mwadui FC yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo la mabao, Salim Aiyee dakika za 33 na 90 na ushei, huku la Geita Gold Mine likifungwa na Baraka Jerome dakika ya 50.
    Kwa matokeo hayo, Mwadui FC inaitoa Geita Gold Mine kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatatu huko Geita.

    Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mabao ya Ally Ramadhani dakika ya 51 na Japhet Makalayi dakika ya 59 yameipa Kagera Sugar ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba SC.
    Kagera Sugar wanaitoa Pamba SC kwa jumla ya mabao 2-0 baada ya sare ya 0-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Jumatatu Uwanja wa Nyamagan mjini Mwanza.
    Mwadui FC ilimaliza nafasi ya 17, Kagera nafasi ya 18 katika Ligi Kuu ya Tanzania iliyomalizika mwezi uliopita, wakati Geita ilishika nafasi ya pili Kundi A na Pamba nafasi ya pili Kundi B kwenye Daraja la Kwanza.
    Ikumbukwe Polisi Tanzania ya Kilimanjaro iliyoongoza Kundi B na Namungo FC ya Lindi iliyoongoza Kundi A zimepanda moja kwa moja Ligi Kuu, wakati African Lyon iliyoshika mkia Ligi Kuu na Stand United iliyomaliza nyuma yao, nafasi ya 19 zimeshuka moja kwa moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR NA MWADUI FC BADO TUPO NAZO LIGI KUU BAADA YA KUZIPIGA PAMBA NA GEITA GOLD PLAY-OFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top