• HABARI MPYA

    Sunday, June 30, 2019

    TFF YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA USAJILI KWA KLABU ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) imetangaza kufunguliwa kwa Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu,Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2019/2020.
    Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo imesema kwamba dirisha litafungwa Julai 31, mwaka huu na hakutakua na muda wa ziada baada ya zoezi hilo kufungwa.
    Taarifa hiyo imesema kwamba ssajili wa mashindano ya CAF kwa Klabu za Simba, Yanga SC, Azam FC na KMC wenyewe utafungwa Julai 10, mwaka huu.

    Baada ya kipindi hicho cha usajili klabu zitakuwa na siku tisa za kusajili kwa kulipa faini ya dola za Kimarekani 250 kuanzia Julai 11 hadi Julai 20, mwaka huu.
    Taarifa imesema kutakuwa na kipindi cha pili cha usajili wa CAF kitakachokua na siku 10 kuanzia Julai 21 hadi Julai 31, 2019 kipindi ambacho watalipa dola 500 na mchezaji ataanza kutumika kuanzia raundi ya pili.
    Simba na Yanga SC wanawakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC na KMC wanawakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho na TFF imesisitiza Klabu zote kufanya usajili kwa wakati.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA USAJILI KWA KLABU ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top