• HABARI MPYA

    Tuesday, June 11, 2019

    MILIMA NA MABONDE SAFARI YA TAIFA STARS MISRI AFCON 2019

    Na Mahmoud Zubeiry, NEW YORK
    HATIMAYE Tanzania itacheza tena Fainali za Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Juni mwaka huu nchini Misri, baada ya kufuzu kama mshindi wa pili wa Kundi L, nyuma ya Uganda Machi 24, mwaka huu.
    Hiyo itakuwa mara ya pili tu Taifa Stars inashiriki AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria, wakati huo bado michuano hiyo ikijulikana kama Fainali za Kombe la Mataifa Huru ya Afrika. Taifa Stars ilikwenda Lagos baada ya kuzitoa Mauritius na Zambia katika raundi mbili tu za mchujo.
    Aprili 16, 1979; Taifa Stars ilifungwa 3-2 na Mauritius 3-2 mjini Curepipe kabla ya kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano Aprili 29, 1979 mjini Dar es Salaam.
    Agosti 11, 1979; Tanzania ilishinda 1-0 dhidi ya Zambia, bao pekee la kiungo Mohammed ‘Adolph’ Rishard mjini Dar es Salaam kabla ya kwenda kulazimisha sare ya 1-1 na KK Eleven mjini Ndola Agosti 26,  1979 wenyeji wakitangulia kwa bao la Chola dakika ya 43, kabla ya Peter Tino kusawazisha dakika ya 84, hivyo Taifa Stars ikafuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1.
    Na kwenye fainali za Lagos 1980 Tanzania ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Nigeria, Misri na Ivory Coast na ikatolewa raundi ya kwanza tu enzi hizo makundi mawili tu, timu nane zinashiriki tofuati na sasa 24. 
    Machi 8, 1980 ilifungwa 3-1 na Nigeria 3-1 mabao ya wenyeji yakifungwa na Lawal dakika ya 11, Onyedika dakika ya 35 na Odegbami dakika ya 85, huku bao la kufutia machozi la Taifa Stars likifungwa na kiungo Juma Mkambi ‘Jenerali’ (sasa marehemu) dakika ya 54 Uwanja wa Surulere.
    Machi 12, 1980; ilifungwa 2-1 Misri, mabao ya washindi yakifungwa na Hassan Shehata dakika ya 32 na Nour dakika ya 38 huku la Taifa Stars likifungwa na Thuweni Ally dakika ya 86.
    Machi 15, 1980; Taifa Stars ikahitimisha mechi zake za Kundi A kwa sare ya 1-1 na Ivory Coast waliotangulia kwa bao la Koma dakika ya saba kabla ya Thuweni Ally kuisawazishia Tanzania dakika ya 59.
    Kikosi cha Taifa Stars kilichotumika kwenye mechi za kufuzu kiliundwa na makipa; Omar Mahadhi (Simba SC), Juma Pondamali (Pan Africans) na Iddi Pazi (Maji Maji FC).
    Mabeki; Leopold ‘Tasso’ Mukebezi (Balimi FC), Mohammed Kajole (Simba SC), Daudi Salum ‘Bruce Lee’ (Simba SC), Ibrahim Kapenta (KMKM), Jellah Mtagwa (Pan Africans), Leodegar Tenga (Pan Africans) na Salim Ameir (Coastal Union).
    Viungo; Juma Mkambi (Yanga), Hussein Ngulungu (Tumbaku), Mohammmed Rishard Adolph (Pan Africans), Shaaban Katwila (Yanga SC), Omar Hussein (Yanga SC), Thuweni Ally (Simba), George Kulagwa (Simba SC). 
    Washambuliaji; Peter Tino (African Sports), Mohamed Salim (Coastal Union) Shaaban Ramadhani (KMKM). Kocha Mkuu alikuw Ray Gama na Msaidizi wake, Joel Bendera wote.
    Na kikosi kilichoshiriki fainali hizo mjini Lagos kiliundwa na makipa; Athumani Mambosasa (Simba SC), Juma Pondamali (Pan Africans) na Iddi Pazi (Maji Maji FC).
    Mabeki; Leopold ‘Tasso’ Mukebezi (Balimi FC), Mohammed Kajole (Simba SC), Daudi Salum ‘Bruce Lee’ (Simba SC), Ahmad Amasha (Yanga SC), Leodegar Tenga (Pan Africans), Salim Ameir (Coastal Union) na Rashid Iddi ‘Chama’ (Yanga SC).
    Viungo; Juma Mkambi (Yanga), Mtemi Ramadhani (Waziri Mkuu), Hussein Ngulungu (Tumbaku), Mohammed Rishard Adolph (Pan Africans) na Willy Kiango (Mwadui FC). GONGA HAPA KUENDELEA KUSOMA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MILIMA NA MABONDE SAFARI YA TAIFA STARS MISRI AFCON 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top