• HABARI MPYA

    Saturday, June 08, 2019

    AHMAD AACHIWA HURU BAADA KUSHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UFISADI

    RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad ameachiwa huru na Taasisi Kuu ya Kupambana na Rushwa nchini Ufaransa (OCLCIFF).
    Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Mwendesha Mashitaka wa Marseille, Xavier Tarabeux amesema Ijumaa kwamba Ahmad ameachiwa bila kufunguliwa mashitaka.
    Ahmad alitiwa mbaroni Ijumaa nchini Ufaransa ambako alikuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

    Rais wa CAF, Ahmad ameachiwa huru na nchini Ufaransa baada ya kukamatwa akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa FIFA


    Ahmad Ahmad raia wa Madagascar alikamatwa ikiwa siku moja baada ya kuongoza kikao cha kamati ya utendaji ya CAF iliyoamuru kurudiwa kwa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Esperance na Wydad Casablanca baada ya kubainika kuwa ilikuwa na ukiukwaji wa taratibu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AHMAD AACHIWA HURU BAADA KUSHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UFISADI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top