• HABARI MPYA

    Wednesday, June 19, 2019

    YANGA SC YAMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MIWILI BEKI WA KATI WA KMC, ALLY ALLY

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI chipukizi wa kati wa kikataifa wa Tanzania, Ally Ahmed Ally amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC.
    Ally ametambulishwa leo makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam baada ya kusaini mkataba huo akitokea KMC ya Kinondoni aliyoichezea kwa msimu mmoja akitokea Mwadui FC ya Shinyanga.
    Ally anakuwa mchezaji mpya wa tisa kusajiliwa Yanga SC na wa pili tu mzawa baada ya kiungo wa ulinzi, Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar.

    Wengine saba wote ni wa kigeni, Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana), Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia.
    Yanga SC imedhamiria kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, baada ya misimu miwili ya kuzidiwa kete na mahasimu wao, Simba SC.
    Baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu mfululizo 2015, 2016 na 2017, Yanga SC wakapokonywa taji hilo na Simba SC 2018 ambao wamefanikiwa kulitetea 2018.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MIWILI BEKI WA KATI WA KMC, ALLY ALLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top