• HABARI MPYA

    Tuesday, June 11, 2019

    ZAMBIA WABEBA TAJI LA TANO LA COSAFA, WATATU UFUNGAJI BORA

    BAO pekee la Tapson Kaseba limeipa Zambia ubingwa wa michuano ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika, COSAFA 2019 baada ya kuilaza Botswana 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Moses Mabhida juzi.
    Matokeo hayo yanamaanisha Zambia wanabeba taji hilo kwa mara ya tano, sasa wakizidiwa taji moja tu na Zimbabwe wanaoongoza kulichukua mara nyingi.
    Na hilo linakuwa taji la kwanza kwao tangu mwaka 2013 walipobeba kwa mara ya mwishon kabla ya kuja kulikosakosa mara mbili walipoingia fainali na kufungwa.

    Kwa ushindi huo, Zambia wamezawadiwa Randi 500,000, wakati Botswana wameondoka na Randi 250,000 huku washindi wa tatu, Zimbabwe wakipewa Randi 150,000, Leostho Randi 125,000 kwa kumaliza nafasi ya nne, wakati washindi wa fainali ya  Plate, Afrika Kusini wamepata Randi 100,000. 
    Baada ya mechi hiyo, Mmalawi Gerald Phiri Jr. alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano akizawadiwa Randi 20,000, kipa wa Zambia, Mwange akishinda tuzo ya Kipa Bora wa Mashindano na kupewa pia kiasi hicho cha fedha.
    Na Randi 20,000 nyingine za Ufungaji Bora watagawana wachezaji watatu, Wamalawi wawili Phiri Junior na Mhango na mshambuliaji wa Mauritius, Ashley Nazira ambao kila mmoja alifunga mabao matatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMBIA WABEBA TAJI LA TANO LA COSAFA, WATATU UFUNGAJI BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top