• HABARI MPYA

    Sunday, June 30, 2019

    AMUNIKE AJIPA MATUMAINI YA KUPATA MATOKEO MAZURI DHIDI YA ALGERIA KESHO

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Taifa, Mnigeria Emmanuel Amuneke anaamini timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 dhidi ya Algeria kuanzia Saa 4:00 usiku wa kesho Uwanja wa Al- Salam mjini Cairo, Misri.
    Akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa leo, Amuneke amesema kuwa licha ya Algeria kuwa na kikosi kizuri, lakini bado ana matumaini makubwa na vijana wake kuwa watafanya vizuri katika mchezo huo wa mwisho wa kundi C.
    “Tumecheza na Algeria mara kadhaa, nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam tuliocheza tukafungwa 2-0 na baadaye tukaja kucheza nao tukatoka nao 2-2, nakumbuka pia walikuja wakatufunga bao 7-0, lakini hiyo yote ni historia,”alisema na kuongeza:

    Emmanuel Amuneke anaamini Taifa Stars itafanya vizuri dhidi ya Algeria kesho mjini Cairo

    “Kwa sasa hivi tunachokitazama ni namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo miwili iliyopita na kufanya maamuzi sahihi tunapokuwa na mpira. Kwa hiyo Jumatatu ni ukurasa mwingine na ni safari nyingine kwa Tanzania na Algeria na hauwezi kutabiri nani atakuwa mshindi, kwa hiyo tutaingia uwanjani kupambana na kusaka pointi tatu,”.
    Taifa Stars itashuka dimbani kupambana na Algeria baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa bao 2-0 na mchezo wa pili dhidi ya Kenya ulioisha kwa Kenya kuibuka na ushindi wa bao 3-2.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMUNIKE AJIPA MATUMAINI YA KUPATA MATOKEO MAZURI DHIDI YA ALGERIA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top