• HABARI MPYA

    Thursday, June 27, 2019

    MISRI NA NIGERIA ZAWA ZA KWANZA KUTINGA 16 BORA AFCON 2019

    MISRI na Nigeria zimefungua milango ya hatua ya 16 Bora ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 baada ya ushindi dhidi ya wapinzani wao Jumatano usiku.
    Nigeria ‘Super Eagles’ ilikuwa ya kwanza kutinga hatua ya mtoano baada ya kuichapa 1-0 Guinea bao pekee la beki wa Leganes ya Hispania, Kenneth Josiah Omeruo dakika ya 73 Uwanja wa Alexandria nchini Misri katika mchezo wa Kundi B.
    Maana yake, timu ya kocha Mjerumani mwenye umri wa miaka 65, Gernot Rohr inafikisha pointi sita katika mchezo wa pili ikiendelea kuongoza Kundi B mbele ya Madagascar na Guinea zenye pointi moja kila moja, wakati Burundi haina pointi.
    Nayo Misri ikaichapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 2-0, mabao ya Ahmed El Mohamady dakika ya 25 na Mohamed Salah dakika ya 43 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
    Mafarao sasa wana pointi sita baada ya mechi mbili, wakiendelea kuongoza Kundi A wakifuatiwa na Uganda wenye pointi nne baada ya sare ya 1-1 na Zimbabwe leo, wakati DRC inashika mkia ikiwa haina na pointi na imekwishatolewa.
    Mshambuliaji wa Simba SC ya Tanzania, Emmanuel Okwi alianza kuwafungia Uganda dakika ya 12, kabla ya kiungo wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, K. Billiat kuwasawazishia Zimbabwe dakika ya 40.
    Uganda sasa itahitaji hata sare kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Misri ili kwenda hatua ya mtoano iipiku Zimbabwe.
    MICHUANO hiyo itaendelea Alhamisi kwa mechi tatu, Kundi C Madagascar itamenyana na  Burundi kuanzia Saa 11:3 jioni mchezo wa Kundi B Uwanja wa 11:30 jioni.
    Mchezo huo utafuatiwa ne mechi mbili za Kundi C, kwanza Senegal na Algeria Saa 20:00 usiku na baadate Saa 5:00 usiku Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo.  Mechi za kwanza Senegal iliichapa 2-0 Taifa Stars 2-0 na Algeria ikaipiga Kenya 2-0. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISRI NA NIGERIA ZAWA ZA KWANZA KUTINGA 16 BORA AFCON 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top