• HABARI MPYA

    Saturday, June 22, 2019

    AMUNIKE AJIPA MATUMAINI TAIFA STARS ITAWAPIGA SIMBA WA TERENGA KESHO CAIRO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Tanzania, Mnigeria Emmanuel Amunike amesema wana imani kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Senegal kesho Uwanja wa 30 June mjini Cairo, Misri.
    Amunike amesema mpaka sasa wameweza kujiandaa kimbinu na kiakili  katika mchezo huo ambao anatambua wanacheza na timu kubwa Barani Afrika, lakini hawana wasiwasi  kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
    “Kikubwa katika mchezo huo, tumejiandaa kisaikolojia na kimbinu ili tuweze kuhakikisha tunapata matokeo mazuri  na tunaamini kesho utakuwa mchezo mzuri wa mashindano na naamini wachezaji wangu wapo kamili kuweza kucheza mchezo huo na wanajua umuhimu wa mchezo huo.


    Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta,alisema Kwamba wanawaheshimu Senegal kwakuwa ni timu kubwa Afrika ,lakini hawatokwenda uwanjani kinyonge.
    “Kikubwa ni kwamba tutakwenda uwanjani,huku tukijua tunaenda kupambana na  timu kubwa na  lazima tupambane uwanjani ili tuwezee kulisogeze jina la nchi yetu,hivyo tunaamini   kabla ya filimbi ya mwisho  kila timu ina nafasi,”.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMUNIKE AJIPA MATUMAINI TAIFA STARS ITAWAPIGA SIMBA WA TERENGA KESHO CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top