• HABARI MPYA

  Friday, August 04, 2017

  SIMBA SC KUREJEA KESHO DAR KWA MAFUNGU

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba SC kinatarajiwa kurejea nchini kesho mchana baada ya kambi ya takriban wiki mbili nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Simba inatarajiwa kuwasili nchini kwa makundi mawili, kundi la kwanza likifika Saa 7:00 mchana na la pili Saa 7:00 kutokana na kukosekana ndege ya kuuchukua msafara wote kwa pamoja.
  Simba SC ambayo Agosti 8, itamenyana na mabingwa wa Rwanda, Rayon Sport Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika kilele cha tamasha la Simba Day, pamoja na mazoezi, nchini Afrika licheza pia mechi mbili za kujipima nguvu.
  Mechi ya kwanza walifungwa 1-0 na Orlando Pirates kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 na mabingwa wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kudini, Bidvest Wits.
  Akizungumza  na Bin Zubeiry Sports – online leo, Ofisa Habari ya klabu hiyo, Hajji Sunday Manara amesema kwamba kikosi kinarejea kikiwa kimeiva na kipo tayari kabisa kwa msimu mpya.
  “Wchezaji wetu wapo fiti kwa mazoezi waliyoyafanya Afrika Kusini walipokwenda kuweka kambi na tumejiandaa vizuri kwenye kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rayon Agosti 8 na kikosi kinatarajiwa kutua kesho majira ya saa saba  mchana na wengine watatua saa saba usiku,”alisema Manara.
  Pamoja na hayo, Manara ametaja pia viingilio katika mchezo wa Agosti 8 kuwa ni Sh.30,000 kwa VIP A, 20,000 kwa VIP B, 15,000 VIP C na 5,000 kwa mzunguko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUREJEA KESHO DAR KWA MAFUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top