• HABARI MPYA

  Saturday, August 12, 2017

  MABINGWA CHELSEA WAKANDAMIZWA DARAJANI, WAPIGWA 3-2 NA BURNLEY

  London, ENGLAND
  MABINGWA watetezi, Chelsea wameanza vibaya Ligi Kuu ya England baada ya kufungwa mabao 3-2 nyumbani, Uwanja wa Stamford Bridge na Burnley.
  Hadi mapumziko, tayari wageni walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Sam Vokes dakika ya 24, Stephen Ward dakika ya 39 na Sam Vokes dakika ya 43.
  Kipindi cha pili, The Blues wakajitutumua na kufanikiwa kupata mabao mawili, yaliyofungwa na Álvaro Morata dakika ya 69 na David Luiz dakika ya 88.

  Kocha wa Chelsea, Antonio Conte akiwa mwenye hasira wakati wa mchezo wa keo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Uwanja wa Vicarage Road, Liverpool ikiambulia sare ya mabao 3-3 mbele ya wenyeji, Watfrod. Mshambuliaji mpya, Mohamed Salam aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 39 kutoka Roma aliifungia Liverpool bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 57, lakini Miguel Britos akaisawazishia Watford dakika ya 90 na ushei.Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 29 na Roberto Firmino kwa penalti dakika ya 55, wakati ya Watford yamefungwa na Stefano Okaka dakika ya nane na  Abdoulaye Doucoure dakika ya 32.
  Mechi nyingine za Ligi hiyo leo; Southampton imetoka sare ya 0-0 na Swansea City Uwanja wa St. Mary's, Crystal Palace imefungwa 3-0 nyumbani Uwanja wa Selhurst Park na Huddersfield Town, Everton imeifunga 1-0 Stoke City, bao pekee la mshambuliaji mpya, Wayne Rooney dakika yab 46 Uwanja wa Goodison Park na West Bromwich Albion imeichapa 1-0 AFC Bournemouth, bao pekee la Ahmed Hegazi dakika ya 31 Uwanja wa The Hawthorns.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINGWA CHELSEA WAKANDAMIZWA DARAJANI, WAPIGWA 3-2 NA BURNLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top