• HABARI MPYA

  Saturday, August 05, 2017

  JULIO AREJESHWA KUGOMBEA TFF, WANNE WAENGULIWA KWA SKENDO YA TAKUKURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKATI Kamati ya Uchaguzi ikimrejesha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwenye uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Agosti 12 mwaka huu mjini Dodoma, wagombea wengine wanne wameenguliwa.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wakili Revocatus Kuuli alisema kamati yake imewaondoa Shaffih Dauda, Elias Mwanjala, Benista Lugola na Ephraim Majige ambao walikuwa wanagombea ujumbe wa kamati ya utendaji.
  Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amerejeshwa kwenye uchaguzi  wa TFF utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma 

  “Tumejidhisha kuwa Julio ni kweli alisoma Kinondoni Muslim baada kupata vithibitisho kutoka baraza la mitihani lakini pia tumewaengua wagombea wanne ambao walikamatwa na TAKUKURU hivu karibuni kule Mwanza,” alisema Kuuli.
  Pia Wakili Kuuli kamati yao imewaondoa wagombea hao lakini pia wana haki ya kukata rufaa kabla ya kamati yao kukaa Jumanne ya wiki ijayo kutoa orodha ya mwisho ya wagombea wote ili kuanza kampeni.
  Jumla ya wagombea 74 walichukua fomu huku 58 wakiwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Kanda mbalimbali hivyo kuondolewa wanne wanabaki 54 huku wagombea 10 wakiomba nafasi urais na makamu rais sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JULIO AREJESHWA KUGOMBEA TFF, WANNE WAENGULIWA KWA SKENDO YA TAKUKURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top