• HABARI MPYA

  Sunday, August 13, 2017

  HAJIB AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIICHAPA MLANDEGE 2-0

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Ibrahim Hajib leo amefunga bao lake la kwanza katika timu hiyo ikishinda 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Uwanja wa Amaan, Zanzibar
  Pamoja na kufunga dakika ya 50 akimalizia krosi ya Mzimbabwe Donald Ngoma, Hajib pia leo ametoa pasi ya bao la pili lililofungwa na winga machachari, Emmanuel Mrtin dakika ya 73.
  Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana, kocha Mzambia, George Lwandamina leo alibadilisha wachezaji wote kipindi cha pili, kasoro kipa Ramadhan Awam Kabwili.
  Ibrahim Hajib leo amefunga bao lake la kwanza Yanga ikishinda 2-0 dhidi ya Mlandege Uwanja wa Amaan, Zanzibar

  Na ni mabadiliko aliyoyafanya ndiyo yaliipa ushindi timu yake katika mchezo huo wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Yanga iliingia kwenye mchezo wa leo ikitoka kufungwa 1-0 jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Ruvu Shooting bao la kujifunga la beki mpya, Abdallah Hajji ‘Ninja’.
  Kwa ujumla mchezo wa leo ni wa tatu wa kujipima nguvu kwa Yanga, baada ya Jumamosi ya wiki iliyopita pia kushinda 3-2 dhidi ya Singida United Uwanja wa Taifa.
  Baada ya mchezo wa leo, mapema kesho asubuhi kikosi cha Yanga kitakwenda Pemba kuweka kambi ya kujiandaaa na mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi ijayo.
  Kipindi cha Yanga leo kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul/Hassan Kessy dk46, Mwinyi Mngwali/Gardiel Michael dk46, Pato Ngonyani/Andrew Vincent ‘Dante’ dk46, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Abdallah Hajji ‘Ninja’ dk46, Maka Edward/Saidi Juma ‘Makapu’ dk46, Yussuf Mhilu/Pius Buswita dk46, Raphael Daudi/Thabani Kamusoko dk46, Matheo Anthony/Ibrahim Hajib dk46, Said Mussa/Emmanuel Martin dk46 na Baruan Akilimali/Donald Ngoma dk46. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAJIB AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIICHAPA MLANDEGE 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top