// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARSENAL WAIPIGA CHELSEA KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARSENAL WAIPIGA CHELSEA KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, August 06, 2017

  ARSENAL WAIPIGA CHELSEA KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO

  London, ENGLAND
  TIMU ya Arsenal imefanikiwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2017-2018 wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Chelsea kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Wembley, London.
  Arsenal sasa wanaifikia Liverpool kwa idadi ya kubeba Ngao, mara 15 wote, baada ya Gunners kuchukua pia katika miaka ya 1930, 1931, 1933, 1934, 1938, 1948, 1953, 1991*, 1998, 1999, 2002, 2004, 2014 na 2015.
  Liverpool na Arsenal, zote zinaifutia Manchester United inayoongoza kwa kubeba taji hilo mara 21 katika miaka ya 1908, 1911, 1952, 1956, 1957, 1965, 1967, 1977, 1983, 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011, 2013 na 2016.


  Wachezaji wa Arsenal wakifurahia na taji laoa la Ngao ya Jamii leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  
  Gary Cahill pekee ndiye aliyefunga penalti ya mabingwa wa Ligi Kuu ya England, wakati kipa Thibaut Courtois alipaisha na mshambuliaji mpya, Alvaro Morata aliyesajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 55 kutoka Real Madrid aligongesha nguzo ya lango.
  Waliofunga penalti za washindi wa Kombe la FA ni Theo Walcott, Monreal, Alex Oxlade-Chamberlain na Olivier Giroud.
  Victor Moses alianza kuifungia Chelsea dakika ya 46 akimtungua kipa wa zamani wa The Blues, Petr Cech kutoka umbali wa mita sita, kabla ya Saed Kolasinac kuisawazishia Arsenal kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 82 kufuatia Pedro kumchezea rafu kiungo Mmisri, Mohamed Elneny. Pedro alitolewa
  Kwa kadi nyekundu kwa rafu hiyo.
  Baada ya mchezo huo, maana yake pazia la Ligi Kuu ya England ndiyo limefunguliwa rasmi na michuano hiyo itafuatia wiki ijayo. 
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech; Holding, Mertesacker (Kolasinac 33), Monreal; Bellerin, Elneny, Xhaka, Oxlade-Chamberlain; Welbeck/Nelson dk88, Lacazette/Giroud dk66, Iwobi/Walcott dk66.
  Chelsea: Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Fabregas, Kante, Alonso/Rudiger dk79, Willian/Musonda dk82, Batshuayi/Morata dk74 na Pedro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL WAIPIGA CHELSEA KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top