// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AMIR KHAN AACHANA NA MKEWE KWA KASHFA MITANDAONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AMIR KHAN AACHANA NA MKEWE KWA KASHFA MITANDAONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Friday, August 04, 2017

  AMIR KHAN AACHANA NA MKEWE KWA KASHFA MITANDAONI

  BONDIA Amir Khan ametishia kumuacha mkewe, Faryal Makhdoom kwa madai anatembea na bondia mwenzake wa Uingereza, Anthony Joshua.
  Wawili hao wametoleana kashfa nzito kwenye kwenye Twitter, kila mmoja akimuita mwenzake msaliti wa kimapenzi.
  Bondia huyo wa Bolton, mwenye utajiri wa Pauni Milioni 23 leo mchana amekwenda mbali zaidi baada ya kumtuhumu mkewe huyo kwamba ana mahusiano na bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua.
  Lakini mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 26, akajibu mapigo kwenye mtandao wa kijamii akidai kwamba mumewe ni muongo, kwani yeye ndiye msaliti. 

  Amir Khan (kushoto) akiwa na mkewe, Faryal Makhdoom ambaye wanasema wameachana PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Wanandoa hao walikuwa pamoja mapumzikoni Dubai kusherehekea Faryal kutimiza miaka 26 ya kuzaliwa wiki iliyopita, lakini inafahamika kwamba Faryal baada ya hapo alirejea peke yake England.
  Joshua, mwenye umri wa miaka 27, amepuuza tuhuma hizo kwa kuposti video ya wimbo wa Shaggy uitwao It Wasn't Me.
  Kisha akatweet: "Natumaini nyie mngetatua matatizo yenu, au akaunti imetekwa, kwa sababu hatujawahi kukutana kabisa! Jumlisha nampenda mwanamke wangu BBW #ItWasntMe',"
  Chanzo kutoka familia ya Khan kimesema; "Amir na Faryal wameachana. Yamekwisha. Wamekuwa wana matatizo katika mahusiano yao kwa muda mrefu na walikuwa wanaelekea kutengana,".
  Katika mfululizo wa tweets za leo, bingwa wa zamani wa Olimpiki, Khan ameandika: "Hivyo mimi na mke wangu Faryal tumekubaliana kuachana. Kwa sasa nipo Dubai. Namtakia yeye kila la heri,".
  "Faryal ameondoka mapema. Wakati wote amekuwa akinitajia kiasi gani anataka kuwa na mvulana mwingine, katika watu wote, bondia mwingine. Amehamia kwenye uzito wa juu. Niamini, mimi si aina ya watu wenye wivu. Haina haja ya kunitumia picha ya mwanaume unayezunguza naye. Nimeachaana na familia yangu na marafiki kwa ajili ya huyu Faryal. Siumii, lakini mpiganaji mwingine. Naiweka hadharani. Umeachika. Wanaume kama Joshua wanaweza kula matapishi yangu,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMIR KHAN AACHANA NA MKEWE KWA KASHFA MITANDAONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top