Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya

VAN PERSIE KULIPWA PAUNI 250,000 KWA WIKI MAN CITY

KLABU ya Manchester City inamtaka mfalme wa mabao England, mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie mwenye umri wa miaka 28, na imempa ofa ya mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki katika harakati za kuwania saini yake.
KLABU ya Everton inafuatilia maendeleo ya mchezaji ambaye yuko mbioni kumaliza mkataba wake, Jonas Olsson. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatazamiwa kupewa mkataba mpya katika klabu hiyo ya Midlands.
KLABU ya Arsenal inataka kumsajili mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey, ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika.
KLABU ya Liverpool inamtaka mshambuliaji wa Aston Villa, Darren Bent, mwenye umri wa miaka 28, ambaye anakaribia kuwa fiti tena.
Darren Bent
Bent alifanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu. 
BEKI Carlos Cuellar, mwenye umri wa miaka 30, anatazamia kuondoka Aston Villa baada ya kukandiwa na mashabiki kwenye Twitter, huku mkataba wake wa miaka minne unaisha mwishoni mwa msimu huu na hajapewa ofa ya mkataba mpya.
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson  yuko tayari kupambana na Tottenham kuwania saini ya mchezaji wa  Crewe, kinda mwenye umri wa miaka 18, Nick Powell.
TAARIFA nchini Ufaransa zinasema kwamba, klabu ya Paris St Germain imejipanga kuipiga bao Chelsea katika kuwania saini ya 'muuwaji' wa Napoli, Muargentina Ezequiel Lavezzi, mwenye umri wa miaka 27.

VITA YA FERGIE NA MANCINI

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini hatimaye amesema timu yake iko kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle jana.
KOCHA Sir Alex Ferguson anaamini kwamba kufukuzwa 'kishenzi' kwa kocha Mark Hughes katika klabu ya Manchester City kutaisaidiaklabu yake, Man United kushinda mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England, - kwani City itamenyana na QPR mwishoni mwa wiki ijayo.
WINGA wa Manchester United, Ashley Young amefurahishwa na uteuzi wa Roy Hodgson kuwa kocha wa timu ya taifa ya England, baada ya bkuzungumza na wachezaji wenzake wa timu ya taifa juu yake.
Ashley Young
Young alifunga katika ushindi wa Manchester United wa 2-0 dhidi yaSwansea
KIUNGO Frank Lampard ameiambia Chelsea kwamba, Didier Drogba ni noma na ameitaka klabu hiyo kukubaliana naye juu ya mkataba mpya abaki Stamfrod Bridge.
CHAMA cha Soka England kitairudia tena sheria ya kutumia teknolojia baada ya utata mwingine wa bao kwenye Uwanja wa Wembley. Mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll alifunga bao lililovuka mstari wa goli dhidi ya Chelsea katika fainali ya Kombe la FA, lakini likakataliwa.
BEKI wa Chelsea, John Terry amesema mmiliki wa klabu yao, Roman Abramovich atatakiwa kumkabidhi ukocha wa klabu hiyo, Roberto di Matteo kuwa kocha wa kudumu kama ataiwezesha timu kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
KOCHA wa Liverpool, Kenny Dalglish amesema kwamba atajadili mustakabali wake Anfield na wamiliki wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

PODOLSKI ASINDIKIZWA NA POLISI

MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Lukas Podolski alilazimika kusindikizwa na polisi kutoka uwanjani, Cologne baada ya mechi ya mwisho na klabu yake ya sasa kutokana na hasira za mashabiki kwa kitendo chake cha kuhama.