• HABARI MPYA

    Friday, May 11, 2012

    ALAN PARDEW KOCHA BORA ENGLAND


    Football | Barclays Premier League

    Alan Pardew

    KOCHA wa Newcastle, Alan Pardew ameshinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya England, baada ya kufanya mambo makubwa akiwa na Magpies akiiwezesha kuwania kumaliza ndani ya Top-Four.
    Newcastle ilitarajiwa kusota msimu huu, baada ya kuondoka kwa Kevin Nolan na Joey Barton, ambao walimfuatia mshambuliaji Andy Carroll aliyeondoka Januari mwaka jana kujiunga na Liverpool.
    Pamoja na hayo, kuteuliwa katika mazingira ya utata kwa Pardew kuchukua nafasi ya Chris Hughton Desemba mwaka 2010, kumeisaidia Newcastle kuzinduka na kufanya mavitu, kiasi kwamba bado wamo kwenye kinyang’anyiro cha kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, hatima yao ikiwa itajulikana katika mechi za mwisho Jumapili.




    .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALAN PARDEW KOCHA BORA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top