• HABARI MPYA

  Tuesday, June 06, 2017

  PEPE AAGA REAL MADRID, ASEMA ANATAKIWA ENGLAND NA PSG

  Beki mkongwe, Pepe akiwa ameinua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumamosi baada ya kulitwaa kwa mara ya tatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  WASIFU WA PEPE 

  Maritimo (2002-04): Mechi 66, mabao 3 
  Porto (2004-07): Mechi 88, mabao 8 
  Real Madrid (2007-17): Mechi 334, mabao 15 
  Ureno (2007-): Mechi 82, mabao 4
  MATAJI: Primeira Liga x2, La Liga x 3, Kombe la Mfalme x2, Ligi ya Mabingwa x3, Klabu Bingwa ya Dunia x2 na Euro 2016 
  NYOTA wa Real Madrid, Pepe amethibitisha anaondoka katika klabu hiyo baada ya miaka 10 na hiyo ni kufuatia kutofautiana na kocha Zinedine Zidane.
  Beki huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 34, amesema ana ofa kutoka klabu za England wakati pia Paris Saint-Germain imekuwa ikimfuatilia kwa muda.
  "Sitaki kumlaumu mtu yeyote. Alichokifanya Zidane na Real Madrid ni cha kuvutia, lakini kuna vitu sivielewi. Sijamuaga Zidane kwa sababu Zidane na Real Madrid walijua nimeondoka kabla sijafanya hivyo,"alisema Pepe.
  Pepe amecheza mechi 334 tangu amejiunga na klabu hiyo kutoka Porto ya kwao, Ureno kwa dau la Pauni Milioni 25.5 mwaka 2007, lakini kwa sasa akina Raphael Varane na Nacho wamepokonywa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza pamoja na Sergio Ramos kama mabeki wa kati.
  "Ni dhahiri kwamba sitaendelea Real Madrid," amethibitisha na mkataba wake ndiyo unamalizikia.
  Pepe ni mshindi wa taji la Euro 2016 akiwa na Ureno, lakini amezaliwa na kukulia Brazil kabla ya kuhamia Ulaya akiwa ana umri wa miaka 18.
  Alijenga ukuta imara Real Madrid kwa pamoja na Ramos Uwanja wa Bernabeu na ataondoka akiwa ameshinda mataji matatu ya La Liga, matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya Kombe la Mfalme na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia akiwa na vigogo wa Hispania.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PEPE AAGA REAL MADRID, ASEMA ANATAKIWA ENGLAND NA PSG Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top