Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Said Mussa akimtoka kwa chenga ya hatari beki wa Tusker ya Kenya, Collins Shivachi hadi kiatu kikamvuka katika mchezo wa SportPesa Super Cup jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Yanga ilishinda kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90
Kiungo huyo aliyekuwamo kwenye kikosi cha timu ya vijana ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki michuano ya Afrika mwezi uliopita nchini Gabon alimtesa mno beki huyu wa Harambee Stars, timu ya taifa ya Kenya
Ikafika wakati ikabidi Collins Shivachi ajaribu kumshika Said Mussa ili kumtuliza
Lakini bado kijana alijinasua na kuendeleza safari yake
Hapa kijana anajaribu kujinasua baada ya kushikwa jezi na Shivachi
Mtu mzima wa Kenya ikabidi acheze hadi rafu kujaribu kumpokonya mpira kinda wa Jangwani
Lakini dogo miguu yake kama ina sumaku inayonasa mpira
Aliinuka na akachukua mpira wake na kuanza kuondoka nao
Jitihada za Mkenya kujaribu kumzuia kijana huyo hazikufanikiwa
Alijaribu kumvuta tena jezi, lakini hakufanikiwa kijana akaambaa na mpira na kuacha mashabiki wakimpigia makofi mengi jukwaani
Invincibles This Week: Two draws, but two to go...
-
Take a look at what was going on around the world and on the pitch 20 years
ago this week during our Invincibles campaign
19 minutes ago
0 comments:
Post a Comment