• HABARI MPYA

  Saturday, June 10, 2017

  PELE: NI KICHEKESHO KUMFANANISHA DYBALA NA MARADONA

  GWIJI wa Brazil, Pele amesema ni kichekesho kumuita mshambuliaji wa Juventus na Argentina, Paulo Dybala ni Diego Maradona mpya.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa ni mmoja wacheza gumzo kubwa Ulaya wenye umri mdogo baada ya kujiunga na Kibibi Kizee cha Turin kutoka Palermo mwaka 2015.
  Dybala amefunga mabao 30 kwa misimu yake miwili ya kucheza Serie A, akishinda mataji katika misimu yote pamoja na kuisaidia timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa.
  Gwiji wa Brazil, Pele (kulia) amesema ni kichekesho kumuita Dybala ni Diego Maradona mpya (kushoto) PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Pamoja na hayo, vigogo hao wa Italia walisambaratishwa na Real Madrid mjini Cardiff kwa kufungwa 4-1 huku mashabiki wakimponda kinda huyo baada ya kucheza ovyo.
  Na akatawala kwenye midomo ya watu baada ya kucheza ovyo pia jana licha ya Argentina kushinda 1-0 dhidi ya Brazil.
  "Si mzuri kama watu wanavyosema,"amesema mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu.
  "Wanasema atakuwa Maradona mwingine, lakini kitu pekee anachofanana na naye ni kutumia mguu wa kushoto tu,"amesema Pele.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PELE: NI KICHEKESHO KUMFANANISHA DYBALA NA MARADONA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top