• HABARI MPYA

    Thursday, June 08, 2017

    GHANA WAITUMIA SALAMU ETHIOPIA KUFUZU AFCON

    TIMU ya taifa ya Ghana, Black Stars jana imeifunga timu ya Daraja la Kwanza, Asokwa Deportivo mabao 6-1 katika mchezo wa kujipima jioni.
    Kocha Mkuu, Kwasi Appiah alitumia vikosi tofauti kila kipindi katikaa mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Baba Yara.
    Jordan Ayew alianza kufunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Samuel Sarfo dakika ya 23, kabla ya Winful Cobbinah kumsetia Frank Acheampong kufunga la pili dakika sita kabla ya mapumziko.
    Kipindi cha pili kiilingia kikosi kipya na kikaribishwa kwa bao la mapema na kufanya mchezo uwe 2-1 baada ya dakika mbili.
    Washambuliaji pacha, Raphael Dwamena na Majeed Waris kila akafunga mabao mawili katika kipindi hicho.
    Waris alianza kufunga kiulaini dakika ya 51 baada ya Dwamena kuwatoka mabeki wawili kabla ya kumpasia mpira mshambuliaji wa Lorient.
    Kisha Dwamena akafunga bao lake la kwanza akimalizia kazi nzuri ya Lumor Agbenyenu dakika ya 65.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akamsetia tena Waris dakika ya 69 kabla ya kwenda kufunga mwenyewe mawili dakika moja kabla ya mchezo kumalizika.
    Black Stars inajiandaa kwa mchezo wa kwanza wa Kundi G dhidi ya Ethiopia kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019. Walya Antelopes wanatarajiwa kuwasili Ghana leo usiku tayari kwa mechi ya Jumapili.
    Vikosi vya Black Stars jana:
    Kipindi cha kwanza; Joseph Addo - Samuel Sarfo, Daniel Darkwah, Rashid Sumaila, Jerry Akaminko, Isaac Sackey, Yaw Yeboah, Afriyie Acquah, Jordan Ayew, Winful Cobbinah, Frank Acheampong
    Kipindi cha apili; Richard Ofori - Harrison Afful, Lumor Agbenyenu, Danirl Amartey, John Boye/70' Nicholas Opoku, Ebenezer Ofori, Andre Ayew, Thomas Partey, Majeed Waris, Raphael Dwamena, Thomas Agyepong
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GHANA WAITUMIA SALAMU ETHIOPIA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top