• HABARI MPYA

  Tuesday, August 15, 2017

  KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA YANGA 7,000 JUMATANO TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga Jumatano ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa Sh. 7,000 kwa majukwaa ya rangi ya bluu na kijani.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba sehemu ya VIP ‘A’ kiingilio kitakuwa ni Sh 25,000; VIP ‘B’ na ‘C’ Sh 20,000 wakati viti vya Rangi la Chungwa watu wataketi kwa Sh 10,000.
  Lucas amesema tiketi zimeanza kuuzwa leo ili kuwapa fursa wadau wa mpira wa miguu kununua mapema kujipeusha na usumbufu.
  Mchezo wa Ngao ya Jamii huwakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao kwa msimu uliopita ni Yanga na washindi wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambao ni kwa sasa ni Simba.
  Timu mbili, watani wa jadi katika soka ya Tanzania zipo visiwani Zanzibarkwa kambi za maandalizi ya mchezo huo, Yanga wakiwa Pemba na Simba wakiwa Unguja. Na Lucas amesema kwamba maandalizi ya huo yanakwenda vema kabisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA YANGA 7,000 JUMATANO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top