Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
KIKOSI chenye wachezaji 20 cha timu ya taifa (Taifa Stars) kinaondoka nchini kesho alfajiri kwenda Bujumbura, Burundi huku kocha wa timu hiyo, Mholanzi Mart Nooij akiahidi kulipa kisasi cha kufungwa 3-0 na timu ya taifa hilo katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya 'Etamba Murugamba' itakayopigwa nchini humo Jumapil.
Katika mechi iliyopita ya kirafiki iliyozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 26, mwaka huu, kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kimefinyangwafinyangwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kulazimisha wacheze waanze wachezaji watano wa 'maboresho', kililala 3-0 dhidi ya Warundi na kuharibu pilau la sherehe zilizokuwa zimefana za miaka 50 ya Muungano.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuagwa kwa Taifa Stars, Nooij alisema amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha kinaibuka na ushindi ilki kulipa kisasi cha kufungwa nyumbani na pia kujihakikishia kupanda katika viwango vya soka vya kimataifa vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
"Ninatambua Burundi ina wachezaji wazuri na wa kimataifa kina (Amisi) Tambwe (Pierre) Kwizera na (Didier) Kavumbagu lakini kwa kikosi tunachokwenda nacho, tuna uhakika wa kushinda ugenini na kulipa kisasi maana walitufunga kwetu," alisema Nooij.
Aliwataja wachezaji 20 anaokwenda nao Bunjumbura kuwa ni pamoja na makipa Mwadin Ally (Azam FC) na Deogratias Munishi 'Dida' (Yanga).
Wengine ni Shomari Kapombe (Azam FC), Oscar Joshua (Yanga), Said Morad (Azam FC), Nadir Haroub 'Canavaro' (Yanga) ,Kelvin Yondani (Yanga), Joram Mgeveke (aliyesajiliwa Simba kutoka kikosi cha Maboresho ya Taifa Stars) ,Simon Msuva (Yanga) ,Erasto Nyoni (Azam FC), Himid Mao (Azam FC), Amri Kiemba (Simba), Haruna Chanongo (Simba), Salum Abubakary 'Sure Boy' (Azam FC), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya in the Qatar), Hamis Mcha (Azam FC), Juma Luizio (Zesco FC, Zambia), Mrisho Ngasa (Yanga), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (wote TP Mazembe, DRC).
Nooij alisema mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor', beki kisiki Agrrey Morris na kipa 'nuksi kwa Yanga', Aishi Manula wameachwa katika msafara wa Burundi kwa sababu mbalimbali zikiwamo majeraha na kutokuwa na uhakika wa kucheza Jumapili.
Alisema Bocco na Morris ni majeruhi huku akieleza kuwa makipa Dida na Mwadini wanatosha kwa mechi hiyo, hivyo haoni sababu ya kwenda na Manula.
Taifa Stars itaingia uwanjani mwishoni mwa wiki ikiwa na kumbukumbu ya kutolewa na Zimbabwe kwenye mbio za kuwania kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika Morocco mwakani.

![]() |
| Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij kushoto na Msaidizi wake, Salum Mayanga |

.png)
0 comments:
Post a Comment