• HABARI MPYA

    Sunday, September 28, 2014

    RAMSEY, WILSHERE NA ARTETA WOTE NJE WIKI AU ZAIDI ARSENAL BAADA YA KUUMIA JANA DHIDI YA SPURS

    KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mikel Arteta wote watakuwa nje wiki ijayo- maana yake majeruhi hao wataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray Jumatani. 
    watatu hao wote wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea Jumapili ijayo, baada ya kuumia jana katika sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur Uwanja wa Emirates.
    Wenger amesema: "Sifahamua muda mrefu kiasi watakuwa nje, lakini watakosekana wiki ijayo. Nafikiri Ramsey ni nyama (maumivu), na Arteta ni misuli ya nyuma ya mguu. Wilshere ni kifundo cha mguu,"amesema.
    Pigo; Kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey akitolewa nje jana baada ya kuumia dhidi ya Spurs
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAMSEY, WILSHERE NA ARTETA WOTE NJE WIKI AU ZAIDI ARSENAL BAADA YA KUUMIA JANA DHIDI YA SPURS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top