• HABARI MPYA

    Wednesday, September 24, 2014

    SHUTI LA MITA 30 LA CLYNE LAING'OA ARSENAL KOMBE LA LIGI

    ARSENAL imefungwa mabao 2-1 na Southamtpon katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Emirates.   
    Alexis Sanchez alitangulia kuwafungia Gunners  dakika ya 14 kwa mpira wa adhabu, kabla ya Dusan Tadic kusawazisha dakika sita baadaye kwa penalty, kufuatia Tomas Rosicky kumchezea rafu Sadio Mane. 
    Mshindi wa mechi; Nathaniel Clyne akiifungia Southampton bao la ushindi jana
    Nathaniel Clyne akaifungia Southampton bao la ushindi kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 40 katika mchezo ambao kiungo anayetoka kwenye majeruhi wa Arsenal, Abou Diaby alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu Machi 2013.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Bellerin/Akpom dk86, Chambers, Hayden, Coquelin, Rosicky, Diaby/Cazorla dk67, Campbell/Oxlade-Chamberlain dk71, Wilshere, Podolski na Sanchez. 
    Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Gardos, Targett/Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Mane/Long dk72, Davis, Tadic na Pelle.
    Jack Wilshere passes the ball away from a Sadio Mane tackle. The England star was part of a strong attacking line-up fielded by Arsene Wenger 
    Jack Wilshere akijaribu kuondosha mpira mbali ya Sadio Mane katika mchezo wa jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHUTI LA MITA 30 LA CLYNE LAING'OA ARSENAL KOMBE LA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top