• HABARI MPYA

    Tuesday, September 23, 2014

    FRANK DOMAYO, BOCCO WAANZA MAZOEZI WIKI IJAYO AZAM FC…KIMWAGA AMEKWISHAANZA MDOGOMDOGO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Frank Domayo ataanza mazoezi mepesi Oktoba 1, mwaka huu baada ya kumaliza muda wa mapumziko kufuatia kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja.
    Domayo aligundulika kuchanika vibaya nyama za paja, baada tu ya kusajiliwa na Azam FC Juni mwaka huu, kufuatia kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC.
    Kufuatia hali hiyo, alipelekwa Afrika Kusini alikofanyiwa opersheni na kutakiwa kupumzika kwa miezi mitatu- na sasa yuko tayari kuanza jaribio la kurejea uwanjani.
    “Nitaanza mazoezi tarehe moja, najisikia vizuri kabisa kwa sasa, kama mambo yatakwenda vizuri natarajia kuanza kucheza labda kuanzia mwishoni mwa mwa mwezi ujao,”amesema.
    Domayo kulia alipokuwa na Kimwaga Afrika Kusini kwa ajili ya operesheni

    Aidha, winga Joseph Kimwaga akiyekwenda kufanyiwa upasuaji pamoja na Domayo, naye ameanza mazoezi mepesi tangu mwishoni mwa wiki.
    Kimwaga aliumia goti mwaka jana katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya kuibuka vizuri kikosi cha kwanza cha Azam kufuatia kupandishwa kutoka akademi.
    Amekuwa nje kwa muda wote akijaribu kutibiwa hapa nyumbani bila mafanikio kabla ya kupelekwa Afrika Kusini, naye sasa anajaribu kurudi tena uwanjani.
    Umaarufu wa Kimwaga ulikuja baada ya kuifungia Azam FC bao la tatu katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita. 
    Kwa upande mwingine, mshambuliaji John Raphael Bocco aliyeumia katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya El Merreikh ya Sudan mwezi uliopita, naye anatarajiwa kuanza mazoezi mapema wiki ijayo.
    John Bocco ataanza mazoezi wiki ijayo

    Tayari majeruhi mwingine wa muda mrefu wa Azam FC, Waziri Salum ameanza mazoezi tangu mwishoni mwa wiki.      
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FRANK DOMAYO, BOCCO WAANZA MAZOEZI WIKI IJAYO AZAM FC…KIMWAGA AMEKWISHAANZA MDOGOMDOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top