• HABARI MPYA

    Wednesday, September 24, 2014

    SUAREZ AFUNGA MAWILI BARCA B IKIUA 5-0 MECHI YA KIRAFIKI

    MSHAMBULIAJI Luis Suarez amefunga mabao mawili akiwa na jezi yaBarcelona kwa mara ya pili, timu B ikiitandika 5-0 timu ya taifa ya vijana ya Indonesia chini ya miaka 19.
    Nyota huyo wa Uruguay na mchezaji mwenzake mpya, Thomas Vermaelen – ambaye pia alifunga walicheza mechi hiyo ya Barca B kujiweka fiti kabla ya kuanza kuchezea kikosi cha kwanza.
    Suarez haruhusiwi kuchezea Barca mechi za mashindano hadi Oktoba 24 atakapomaliza kutumikia adhabu yake ya kumng’ata Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunia. 
    Suarez anatarajiwa kuanza kuitumikia rasmi Barcelona katika mechi na Real Madrid Oktoba 24 kwenye La Liga.
    Winga David Babunski na Bicho nao pia walifunga kukamilisha mabao hayo matano Uwanja wa Barcelona Complex.
    Luis Suarez akiichezea Barcelona B dhidi ya makinda wa Indonesia, mechi ambayo alifunga mabao mawili 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AFUNGA MAWILI BARCA B IKIUA 5-0 MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top