• HABARI MPYA

    Thursday, September 04, 2014

    WACHEZAJI WAPYA MAN UNITED WANAISHI KATIKA HOTELI LA KIFAHARI LA BEI MBAYA

    WACHEZAJI wapya wa Manchester Unite wanaishi katika hoteli ya kifahari ya nyota tano, Lowry mjini Manchester wakati wakisubiri kupatiwa nyumba za kuishi.
    Wachezaji hao Radamel Falcao, Angel di Maria, Daley Blind, Ander Herrera, Luke Shaw na Marcos Rojo wamejiunga na klabu hiyo msimu huu kutoka klabu tofauti.
    Hoteli hiyo inaonekana kuwa kipenzi na mabosi wa United, kwani hata kocha Louis Van Gaal aliishi hapo kwa muda alipowasili kabla ya kupatiwa nyumba. 
    Nyota tano: Marcos Rojo (kushoto) ni miongoni mwa wachezaji wapya wa United wanaoishi katika hoteli hiyo
     

    BEI YA VYAKULA LOWRY

    Supu: Lobster Bisque - Pauni 8.00
    Starter: Dressed East Coast Crab - Pauni 13.50
    Main: Cote de Boeuf - Pauni 38.00
    Side: Garlic Roasted Tomatoes - Pauni 3.50 
    Dessert: Dark Chocolate Fondant - Pauni 8.00 
    Chumba cha suit kwa ajili ya familia katika hotel ya Lowry gharama yake ni Pauni 789 kwa siku, chumba cha kawaida cha watu wawili Pauni 252wakati chumba cha kawaida cha mtu mmoja kwa siku Pauni 248.
    Katika hoteli hiyo ya kifahari, Manchester United inaingia gharama kubwa kwa ajili ya wachezaji hao wa huduma nyingine wanazopatiwa za bei mbaya kama vyakula na vinywaji.
    Five-star: The Lowry hotel has enjoyed as much success as Manchester United with over 60 awards
    Nyota tano: Hoteli ya Lowry ni yenye had hi kubwa

    BEI ZA VYUMBA HOTELI YA LOWRY... 

    Suti ya Familia - Pauni 748 kwa siku
    Chumba ha watu wawili- Pauni 252 kwa siku
    Chumba cha mtu mmoja- Pauni 248 kwa siku 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WAPYA MAN UNITED WANAISHI KATIKA HOTELI LA KIFAHARI LA BEI MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top