• HABARI MPYA

    Friday, September 26, 2014

    FIFA YAPIGA STOP MAGUMASHI YA UMILIKI WA TATU KWA MCHEZAJI...KIKOSI KAZI CHAUNDWA KUUNDA SHERIA MPYA

    KAMATI Kuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imepiga kura kuzuia umiliki wa tatu wa wachezaji ambao umekuwa ukiruhusu wawekezaji wa nje kunufaika na uhamisho.
    Rais wa FIFA, Sepp Blatter amesema kikosi kazi kitaandika sheria sasa ya kufuata.
    Uamuzi huo wa leo ni ushindi wa kisiasa kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na Rais wake, Michel Platini, ambaye amekuwa akirudia kuitaka FIFA kuchukua hatua.
    Kamati Kuu ya FIFA, ikiongozwa na Rais Sepp Blatter, imepiga kura kuzuia umiliki wa tatu kwa wachezaji 
    Manchester City's £32m purchase of Eliaquim Mangala from Porto in the summer was one example of a deal reprotedly involving third-party ownership
    Usajili wa Manchester City wa Pauni Milioni 32 kwa Eliaquim Mangala kutoka Porto msimu huu ni moja ya mifano ya dili za umiliki wa pande tatu
    Manchester United's purchase of defender Marcos Rojo reportedly involved buying out a third-party owner
    Usajili wa Manchester United pia kwa beki Marcos Rojo uliripotiwa kuhusisha panda tatu za wamiliki

    Umiliki wa panda tatu ni maarufu kwa mawakala, wawekezaji na klabu za Latin Amerika, Hispania na Ureno, lakini tayari umezuiwa nchini England.
    Licha ya hivyo, klabu kadhaa za Ligi Kuu England zimeripotiwa kununua wachezaji kwa wamiliki wa tatu pia ili kufanikisha nyota zilizowasajili msimu huu. 
    Eliquim Mangala aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 32 kutoka Porto kwenda Manchester City, Marcos Rojo Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon kwenda Manchester United na Lazar Markovic Pauni Milioni 20 kutoka Benfica kwenda Liverpool wote waliripotiwa kununuliwa kwa wamiliki watatu.
    UEFA inasema uhamisho wa aina hiyo unazigharimu klabu fedha nyingi wakati wa kununua wachezaji na wakati mwingine unawakwamisha wachezaji wanapotaka kununuliwa na klabu ambazo haziko tayari kulipa kwa wamiliki watatu- na haina msaada kwa mchezaji ambaye anaachwa na klabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIFA YAPIGA STOP MAGUMASHI YA UMILIKI WA TATU KWA MCHEZAJI...KIKOSI KAZI CHAUNDWA KUUNDA SHERIA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top