• HABARI MPYA

    Saturday, September 20, 2014

    REAL MADRID YAPIGA NANE, RONALDO ATIMIZA HAT TRICK 23 LOS BLANOCS

    KLABU ya Real Madrid imeifumua Deportivo la Coruna mabao 8-2 katika La LIga Uwanja wa Riazor jioni hii, Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 23 kwa Los Blancos.
    Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika za 29, 41 na 78, wakati mabao mengineya Real yamefungwa na James Rodriguez dakika ya 36, Gareth Bale dakika ya 66 na 74 na Javier Hernandez ‘Chichairto’ dakika ya 88 na 90.
    Deportivo ilipata mabao yake ya kufutia machozi kupitia kwa Haris Medunjanin na Jose Verdu Nicolas.
    Kikosi cha Real kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Ramos, Varane, Marcelo, Modric/IIaramendi, Kroos, Bale/Hernandez, James, Ronaldo na Benzema/Isco.
    Deportivo: Lux, Laure, Diakite, Sidnei, Luisinho, Bergantiños, Medunjanin, Juanfran/Juan Dominguez, Farina/Toche, Cuenca na Postiga/Cavaleiro.
    Ronaldo akipongezana na Rodriguez baada ya kufunga leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL MADRID YAPIGA NANE, RONALDO ATIMIZA HAT TRICK 23 LOS BLANOCS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top