• HABARI MPYA

    Wednesday, September 24, 2014

    TORRES AFUFUA MAKALI YA KUFUNGA SERIE A MILAN IKITOA SARE NA KITIMU KILICHOPANDA

    MSHAMBULIAJI Fernando Torres amefunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza kuanza AC Milan timu yake hiyo mpya ikitoa sare ya 2-2 na Empoli iliyopanda Serie A msimu huu.
    Baada ya mabao ya mapema ya Lorenzo Tonelli na Manuel Pucciarelli, Torres akaifungia Milan kwa kichwa dakika ya 43 na mwanasoka wa kimataifa wa Japan, Keisuke Honda akasawazisha kwa shuti la mbali dakika ya 58.
    Milan alipata nafasi ya kuifungia Milan bao la ushindi wakati Torres, aliyejiunga na timu hiyo mwezi uliopita kwa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea, alimsetia Jeremy Menez dakika ya 62, lakini Mfaransa huyo akagongesha mwamba.
    Fernando Torres akishangilia bao lake la kwanza AC Milan jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TORRES AFUFUA MAKALI YA KUFUNGA SERIE A MILAN IKITOA SARE NA KITIMU KILICHOPANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top